WHATSAPP, SMARTPHONE NA UCHUMI WETU.
Rasilimali kuu mbili, zenye thamani kubwa ambazo tumepewa mapema kabisa na Mungu, ni MUDA na AKILI. Hii ni kwa sababu maisha yetu yanategemea MAELEKEZO/MAARIFA na jinsi tunavyotumia MUDA; katika kufuata maelekezo husika.
Leo nimetamani sana kukukaribisha kwenye programu za maarifa mtandaoni. Ni programu [3] ambazo zitaongeza thamani kubwa mno, kwenye sehemu ya matumizi yako ya muda fulani unaoutumia kwenye intaneti; husunan unapotumia simu janja (Smartphone) yako, kwenye messenger ya WhatsApp.
Tunazo programu tatu za maarifa:
№1. UBUNIFU WA GRAPHICS NZURI KWA SMARTPHONE [Na kuziuza kwa wateja waliopo WhatsApp].
№2. KUONGEZA UPATIKANAJI MZURI WA WATEJA KUPITIA WHATSAPP.
№3. KUINGIZA [SEHEMU YA] KIPATO KWA SMARTPHONE NA WHATSAPP.
———————
Bila shaka unayo biashara au unatoa huduma ambayo wahitaji (wateja) wake wengine [wengi] wanapatikana WhatsApp. Kwa sababu hiyo, programu namba mbili: 'Namna nyingine nzuri ya KUONGEZA UPATIKANAJI WA WATEJA KUPITIA WHATSAPP' ina mchango mkubwa wa kukuongezea mwendo na hatua za kukufikisha mbali zaidi.
———————
Lakini pia hata kama hauna jambo unalofanya Mtandaoni, hasa hasa kupitia WhatsApp, linaloweza kukuingizia sehemu nzuri ya kipato chako; programu namba moja (UBUNIFU WA GRAPHIC NZURI KWA SMARTPHONE) inakupa mwanzo na mwendelezo mzuri wa kufanya jambo hilo, yaani ubunifu wa graphics kama vile: posters, flyers, business card, kalenda, makava rahisi ya vitabu na nyingine nyingi—kwa kuwahudumia wahitaji (wateja) wake wanaopatikana WhatsApp. Graphics zinahitajika sana, na watu wengi waliopo WhatsApp ni wahitaji wa graphics.
———————
Vilevile programu namba tatu (Namna ya kuingiza sehemu ya KIPATO KWA SMARTPHONE NA WHATSAPP) inakufaa zaidi, kwa sababu inakupa kujua mambo mengine zaidi, sambamba na hilo la graphics; unayoweza kuyafanya ukiwa na smartphone yako, kifurushi chako cha intaneti, Apps za kufanikisha kazi au huduma husika na sehemu ya muda wako—wa kuwepo mtandaoni. Programu hii inakupa maarifa juu ya huduma na biashara ndogondogo zenye tija, zisizohusisha ulazima wa kukutana ana kwa ana na wateja wako—na zinawezekana kufanyika kupitia WhatsApp. Hii ni kwa sababu utapata uwezo mzuri wa kutengeneza na kuuza baadhi ya bidhaa za kidigitali (Digital/Downloadable Products), zinazohitajika kwa wingi mtandaoni—hususan kwa watu wengi waliopo WhatsApp.
———————
Hivyo basi, wewe unayehitaji kuwafikia watu wengi kupitia WhatsApp; ili wafahamu uwepo wa bidhaa, huduma au biashara yako, programu namba moja ni suluhisho lako. Pia wewe unayehitaji kuanza au kuongeza jambo lingine la kufanya mtandaoni, kwa lengo zuri la kuwahudumia watu waliopo WhatsApp na kuingiza sehemu nzuri ya kipato chako; programu zote zikakufaa kabisa. Unaweza kuamua, uanze na programu gani na umalizie kwa programu ipi.
———————
BEI ZETU:
PROGRAMU №1: UBUNIFU NA UUZAJI WA GRAPHIC NZURI KWA SMARTPHONE.
Tsh 3,500: Kitabu (PDF) & Audio zote.
Tsh 5,000: Kitabu (PDF), Audio za vipengele vyote na kuwepo kwenye kikundi cha WhatsApp [Simplified Graphic Designing], bila ukomo wa muda.
PROGRAMU №2: Namna nyingine nzuri ya KUONGEZA UPATIKANAJI WA WATEJA KUPITIA WHATSAPP.
Tsh 4,500: Kitabu (PDF) pekee.
Tsh 9,000: Kitabu (PDF) na Audio za vipengele vyote.
Tsh 12,000: Kitabu (PDF), Audio za vipengele vyote na kuwepo kwenye kikundi cha WhatsApp [Maximum Sale Via WhatsApp], bila ukomo wa muda.
PROGRAMU №3: NAMNA YA KUINGIZA SEHEMU YA KIPATO KWA SMARTPHONE NA WHATSAPP.
Tsh 3,500: Kitabu (PDF) & Audio zote.
Tsh 7,000: Kitabu (PDF), Audio za vipengele vyote na kuwepo kwenye kikundi cha WhatsApp [e-Businesses Via WhatsApp], bila ukomo wa muda.
———————
Kuna dokumenti zetu (PDF) fupi fupi, kwa kila programu iliyotajwa hapa; zenye ufafanuzi wa utangulizi, na zinapatikana BURE kwa WhatsApp; kwa kuzipakua HAPA [Namba 1][Namba 2][Namba 3], kwa kugusa hayo maneno yenye rangi ya kijani (kwa namba ya programu husika). Dokumenti hizo zinakupa maelekezo muhimu (ya utangulizi), kuhusu programu husika. Uwe huru pia kuuliza lolote (0743517138) kuhusu programu yoyote.
Karibu sana.
___________________
EO Gadgets 77.
+255 743 517 138.
emmanuellibraries@gmail.com
Emmanuel Kimanisha.
___________________
Comments
Post a Comment