NAFASI YA KUMFUATA MTU INBOX KWA MANUFAA MAKUBWA.


Miongoni mwa njia nzuri zitakazokuletea matokeo mazuri sana katika kutangaza biashara au huduma yako, ni kumfuata mtu Inbox. Njia hii inasaidia pia kujenga mahusiano ya uaminifu na uhuru wa mteja kukutafuta yeye mwenyewe hata kwa siku za baadae, anapohitaji bidhaa au huduma yako.

Lakini kuna mambo machache ya kuzingatia, ili jambo hili liwe la manufaa kwako na kwa mtu huyo uliyemfuata inbox. 

Usiingie tu na kumtumia tangazo lako, halafu unaondoka. Ukifanya hivi hautapata matokeo mazuri. Wala usiingie tu, ukamsalimia halafu ukamtumia ujumbe au tangazo lenye maelezo mengi sana kwa wakati mmoja. Nenda kwa jumbe fupi fupi kama nilivyojaribu kutoa mwongozo wa ujumla, hapa chini:

Ujumbe wa kwanza: Msalimie mtu huyo, kwa ujumbe mfupi wa kwanza; mfano: 

'Rafiki, habari yako!'

Ujumbe wa pili: Jitambulishe kwa ufupi; kwa mfano: 

'Bila shaka namba hii ni ngeni kwako, na naomba nijitambulishe kabisa. Naitwa Yavan Kim, napatikana Dar es Salaam.'

Ujumbe wa tatu: Eleza mapema kule ulikoitoa namba yake; mfano: 

'Nilipata mawasiliano yako niliposevu namba zote za washirika wa kikundi cha wasapu cha UPATIKANAJI WA WATEJA KUPITIA WASAPU.' 

Ujumbe wa nne: Eleza lengo lako vizuri; mfano:

'Sababu ya kukufuata Inbox kwa utulivu huu, ni hii: nimeona ni vyema uwe miongoni mwa watu ambao ninahitaji kufahamiana nao ili nafasi inapopatikana iwe rahisi kushirikishana ufahamu, maarifa na taarifa nzuri za kuboresha vile tunavyoishi—kibiashara, kijamii na kiuchumi kwa ujumla.'

Baada ya hapo, mara nyingi atakuuliza kwa kutaka kujua zaidi kuhusu lengo lako. Unatakiwa kumuuliza maswali mengi mazuri, na kutulia katika kumsikiliza yeye zaidi. Katika mawasiliano hayo (unapomsikiliza yeye kwa umakini mkubwa) utaanza kugundua namna nzuri ya kumwambia jambo kuhusu huduma au bidhaa zako.


Hapo sasa, unatakiwa kumshukuru na kuanza kufanya 'Prospecting'. Yaani kuanza kutumia mbinu mojawapo ya kutafuta na kuandaa wateja tarajiwa. Na kwa whatsapp, hususan unapomfuata mtu inbox; unakuwa umetumia mbinu moja inaitwa P2P Sales Prospecting. Kama tunavyojua kuna mbinu kuu tatu, yaani.

1. Business to Business (B2B) Sales Prospecting

2. Business to Customer (B2C) Sales Prospecting

3. Person to Person (P2P) Sales Prospecting.

Kwa leo niishie hapa.

Unaweza pia kujipatia kitabu chetu kizuri chenye maelekezo yote, juu ya namna nzuri mpya iliyopo sasa; katika kutafuta na kuandaa wateja wengi kupitia wasapu. Kitabu hiki kitakupa uwezo kwa kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa wateja wako wa uhakika—kupitia Whatsapp.

Maarifa yake ni kwa ajili ya kuandaa wateja wengi, kupitia wasapu; kwa biashara yoyote uliyonayo na huduma zozote unazozitoa kivyovyote (online/offline).

•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—•••—

  • Angali kava lake, kwa picha, HAPA.
  • Angalia ukurasa wa orodha ya yaliyomo HAPA.
  • Angalia picha ya ukurasa wa utangulizi HAPA.

Karibu sana.

Kinapatikana kwa wasapu; ni PDF kwa Tsh 3,500/-.

Unaweza kukipata leo kwa kunitaarifu Inbox, kwa kuingia HAPA.

MATANGAZO MENGINE:

1. [Kitabu cha PDF] Namna na njia rahisi ya kuanza kuuza maandishi yako mtandaoni: Tsh 2,500 [angalia picha HAPA].

2. [Kitabu na audio] Namna ya kutengeneza Graphics na kuziuza kwa wateja wengi waliopo wasapu: Tsh 4,500 [angalia picha HAPA].

3. Tunakutengenezea matangazo mbalimbali  kulingana na hitaji lako: Tsh 5,000 hadi Tsh 30,000 [anagalia picha HAPA].

4. Tunakutengenezea kalenda ya mwaka 2021 yenye picha zako [Tsh 1,500 softcopy badala ya Tshs 4,500] [angalia picha HAPA].

5. [Kitabu cha PDF] Namna ya kuanza kuingiza sehemu ya kipato chako kwa kufundisha uzoefu au maarifa ya kipaji chako mtandaoni: Tsh 4,000 [angalia picha HAPA].

6. Tunakutengenezea tangazo zuri la audio kwa kuweka ala nzuri za muziki nyuma ya sauti ya mtangazaji: Tsh 5,000/audio sekunde 30 [angalia picha HAPA].

7. Tunakusaidia kuandika kazi zako za maandishi (documents) ya maelezo ya kawaida, kwa haraka (Tsh 350/page) [angalia picha HAPA].

8. KARIBU KWENYE HUDUMA NA PROGRAMU ZETU —MTANDAONI [angalia posti ya ukaribisho HAPA].
••••°°°••••°°°••••°°°••••°°°••••°°°••••°°°••••
ILI KUPATA HUDUMA, PROGRAMU AU KITABU CHOCHOTE KATI YA HIVYO VILIVYOTAJWA HAPO; NJOO INBOX KWA KUFUNGUA HAPA.   




Comments

Popular posts from this blog

KALENDA YAKO [2021] YENYE PICHA ZAKO

HAKUNA LISILOWEZEKANA KATI YA HAYA MAMBO 7.

TENGENEZA KALENDA YAKO YENYE PICHA ZAKO.